MAREKANI: Takriban watu wanne waliuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya mtu aliyejihami kwa bunduki kuliendesha gari katika kanisa la Michigan, kufyatua risasi na kuliteketeza jengo hilo, kabla ya kujiua mwenyewe, polisi wanasema. Maafisa walisema shambulio dhidi ya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huko Grand Blanc, mji ulio umbali wa kilomita 100 kaskazini magharibi mwa Detroit, lilitokea wakati wa ibada ya Jumapili iliyohudhuriwa na mamia ya watu.
Mshukiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Thomas Jacob Sanford, 40, kutoka Burton, Michigan, baadaye aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika eneo la kuegesha magari la jengo hilo. Mamlaka inachunguza tukio hilo kama "kitendo cha vurugu iliyolengwa", lakini wanasema nia bado haijafahamika.