Tanzania, Kyrgyzstan tamko la wino la kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia

SALUM
By -
0


 NEW YORK: TANZANIA na Kyrgyzstan zimesaini tamko la pamoja la kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya pande zote mbili. Tamko hilo limetiwa saini kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mahmoud Thabit Kombo, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kyrgyzstan Ijumaa mjini New York, Marekani.

Aidha, uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili utaongozwa na Mkataba wa Vienna wa Mahusiano ya Kidiplomasia (1961) na sheria nyingine za kimataifa. Akizungumza mara baada ya kusaini tamko hilo, Waziri Kombo aliipongeza Kyrgyzstan kwa uamuzi wake wa kufungua ubalozi Addis Ababa, na kubainisha kuwa ni hatua ya kimkakati ambayo itarahisisha mawasiliano ya moja kwa moja na nchi za Afrika na kuimarisha ushirikiano na Tanzania kupitia Ubalozi wake nchini Ethiopia, ambapo Balozi wake pia amepewa kibali.

Tags:

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default