Yanga yazidi kuimarika jijini Dar

SALUM
By -
0


 Yanga yazidi kuimarika jijini Dar

DAR ES SALAAM: Kocha Mkuu wa Young Africans, Romain Folz ameonyesha imani na maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wiliete Benguela wikiendi hii. 

Mchezo huo umepangwa kutimua vumbi kesho saa 5:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. 

Folz alisema licha ya kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mechi yao ya kwanza, wanaendelea kuwaheshimu wapinzani wao na wanalenga kupata ushindi mwingine ili kuwafurahisha mashabiki wao. 

Kiungo wa Yanga, Aziz Andabwile alibainisha kuwa wachezaji hao wana ari kubwa na nia ya kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kama walivyofanya katika mechi iliyopita kwa lengo la kusonga mbele zaidi kwenye mashindano hayo.

Kwa upande wa Wiliete Benguela, kocha mkuu Bruno Ferry alikiri kuwa mechi itakuwa ngumu, lakini akasisitiza kuwa timu yake haijakata tamaa licha ya kupoteza mechi ya kwanza. 

Mchezaji Mahalatsi Makudubela aliongeza kuwa lengo lao ni kushinda mechi hiyo, akisisitiza kwamba “kila kitu kinawezekana

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default