CCM yawahakikishia wakazi wa Moshi ari ya kuwainua wananchi kiuchumi

SALUM
By -
0


 MOSHI: MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Tanzania Bara, Stephen Wasira, chama tawala, kimejipanga kuona Watanzania wanaendeleza uchumi wa kati ikiwa ni Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030. Akizungumza huko Vunjo mkoani Kilimanjaro vijijini, Wassira alisema serikali chini ya uongozi wa CCM imedhamiria kuwaletea wananchi maendeleo yanayotarajiwa na kuwaonya wale wanaonung’unika na kufikisha ujumbe wa changamoto mbalimbali nchini kwa njia ya maandamano akisema kuwa mambo hayo yamepitwa na wakati na si njia sahihi ya kuwasilisha hoja. Bw Wasira alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kutoka majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, Moshi mjini. Alisisitiza kuwa kuna njia bora na zinazofaa zaidi za kufikisha ujumbe kwa mamlaka zinazofaa, hasa kwa njia za amani. Akifafanua Makamu Mwenyekiti huyo alisema zipo njia bora na sahihi zaidi za kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika hasa kwa njia za amani. PIA SOMA: Mgombea urais wa ADA–TADEA aahidi serikali jumuishi Aidha, alisema wanachotaka Watanzania ni maendeleo na kwamba Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 imedhamiria kuleta maendeleo yanayotarajiwa kwa wananchi. Bw Wasira alisema kuwa ujenzi wa miundombinu muhimu utarahisisha shughuli za kiuchumi na kutoa ajira kwa wananchi. "Watu wanadai reli ya kisasa, kwa sababu katika nchi zinazoendelea, tofauti kati ya nchi zetu na zilizoendelea ni miundombinu. Ukifika unaona barabara pana, na kuna reli ya kasi, hivyo kila kitu kinakwenda haraka," alisema. Aidha, alisema kuwa Ilani ya Chama inaelekeza reli kuunganisha Pugu, Tanga na Arusha kupitia Kilimanjaro

Tags:

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default