KCMC, Kilimanjaro Wonders kujenga viwanja vinne vya daraja la FIFA

SALUM
By -
0


 KCMC, Kilimanjaro Wonders kujenga viwanja vinne vya daraja la FIFA

KILIMANJARO: Kituo cha afya cha Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) kimesaini mkataba na Kituo cha Michezo cha Kilimanjaro Wonders kujenga viwanja vinne vya kisasa vya mpira wa miguu vinavyokidhi viwango vya kimataifa vinavyotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa)

Mradi unalenga kuweka mazingira rafiki ya michezo kwa watoto wenye ualbino, wafanyakazi wa KCMC, wanafunzi, jamaa za wagonjwa, na jamii pana.

Katika hafla ya utiaji saini leo, KCMC iliwakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Prof. Gileard Masenga, na Ofisa Sheria, Rachelly Mboya. Kituo cha Michezo cha Kilimanjaro Wonders kiliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Laurent Kinabo, na Mkurugenzi, Jeffrey Skinner.

Ujenzi wa viwanja hivyo unatarajiwa kuanza mapema Oktoba mwaka huu na unatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya michezo na burudani mkoani humo.

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default