DROO ya CAF Champions League Hatua ya Makundi 2025/2026

SALUM
By -
0


 Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeendesha na kukamilisha Droo ya hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika studio za Mshirika wa CAF Broadcast Partner SuperSport mjini Johannesburg leo Jumatatu ya November 03/2025. Katika droo hiyo timu za RS Berkane na Pyramids FC ambao ni Washindi wa Kombe la Shirikisho na CAF Champions League msimu uliopita wamepangwa 

  • Kundi A Pamoja na Rivers United ya Nigeria na Power Dynamos ya Zambia. Washindi mara 12, Al Ahly ya Misri wamepangwa
  •  Kundi B pamoja na Young Africans ya Tanzania, AS FAR Rabat ya Morocco pamoja na JS Kabylie ya Algeria. 
  • Kundi C wapo Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Hilal SC ya Sudan, MC Alger ya Algeria Pamoja na St Éloi Lupopo ya DR Congo. Washindi mara nne Espérance de Tunis ya Tunisia wanaongoza 
  • Kundi D, pamoja na Simba SC ya Tanzania, Petro de Luanda ya Angola na Stade Malien ya Mali.


Hatua ya Makundi itaanza wikendi ya tarehe 21–23 Novemba 2025, kwa siku mbili za mechi kuchezwa kabla ya kuanza kwa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies CAF Morocco 2025, Kisha kuanza tena wikendi ya tarehe 23-25 ​​Januari 2026. Awamu ya mtoano itaanza tarehe 13 Machi 2026, huku Mshindi akipata zawadi ya dola za Kimarekani 4,000,000, huku washindi wa pili watapata USD 2,000,000.

Makundi Kamili ya CAF Champions League 2025/2026

  •  Kundi A: RS Berkane (Morocco), Pyramids FC (Misri), Rivers United (Nigeria), Power Dynamos (Zambia) 
  • Kundi B: Al Ahly (Misri), Young Africans (Tanzania), AS FAR (Morocco), JS Kabylie (Algeria) 
  • Kundi C: Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Al Hilal (Sudan), MC Alger (Algeria)
  •  Kundi D: Espérance de Tunis (Tunisia), Simba SC (Tanzania), Petro de Luanda (Angola), Stade Malien (Mali) 

Siku za Mechi za CAF Champions League 2025/2026 Hatua ya Makundi

  •  MD1: 21-23 Novemba 
  • MD2: 28-30 Novemba 
  • MD3: 23-25 ​​Januari 
  • MD4: 30 Januari-01 Februari
  •  MD5: 06-08 Februari 
  • MD6: 13-15 Februari

Post a Comment

0 Comments

Post a Comment (0)
3/related/default