Droo ya hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup 2025/2026) imefanyika Leo Jumatatu tarehe 3 November 2025 huko Afrika Kusini. Katika droo hiyo Kutakuwa na Derby ya Misri baada ya Zamalek na Al Masry kupangwa Kundi moja (Kundi D) Pamoja na vigogo wa Afrika Kusini Kaizer Chiefs na timu ya Zambia ZESCO United. USM Alger kutoka Algeria ndio vinara katika Kundi A na wamepangwa na Djoliba AC de Bamako (Mali), Olympique Club de Safi (Morocco) na FC San Pedro (Cote d’Ivoire). Mabingwa mara tatu wa CAF Champions League Wydad Casablanca kutoka Morocco wamepangwa Kundi B Pamoja na AS Maniema (DR Congo), Azam FC (Tanzania) na Nairobi United (Kenya). CR Belouizdad ya Algeria imepangwa na Stellenbosch FC kutoka Afrika Kusini, pamoja na AS Otoho (Congo) na Singida Black Stars (Tanzania) katika Kundi C.
Hatua ya Makundi itaanza wiki ya tarehe 21-23 Novemba kwa raundi mbili kuchezwa kabla ya CAF Africa Cup of Nations Morocco 2025 na mechi hizo zitaendelea tena wiki ya tarehe 23-25 January 2026. Bingwa wa CAF Confederation Cup 2025/2026 atajinyakulia zawadi ya dola milioni 2 huku mshindi wa pili akipokea dola milioni 1. Timu zitakazosonga mbele kutoka hatua ya Makundi zimehakikishiwa kima cha chini zaidi cha dola za Kimarekani 550,000, huku zile zitakazoshika nafasi ya tatu na nne kwenye kundi lao zikipokea dola 400,000.
Makundi Kamili ya Kombe la Shirikisho 2025/2026
- Kundi A: USM Alger (Algeria), Djoliba AC de Bamako (Mali), Olympique Club de Safi (Morocco), FC San Pedro (Cote d’Ivoire)
- Kundi B: Wydad Casablanca (Morocco), AS Maniema (DR Congo), Azam FC (Tanzania), Nairobi United (Kenya)
- Kundi C: CR Belouizdad (Algeria), Stellenbosch FC (Afrika Kusini), AS Otoho (Congo), Singida Black Stars (Tanzania)
- Kundi D: Zamalek (Misri), Al Masry (Misri), Kaizer Chiefs (Afrika Kusini), ZESCO United (Zambia)
- MD1: 21-23 Novemba
- MD2: 28-30 Novemba
- MD3: 23-25 Januari
- MD4: 30 Januari-01 Februari
- MD5: 06-08 Februari
- MD6: 13-15 Februari
