SIMBA Yapangwa Kundi D CAF Champions League 2025/2026
Klabu ya Simba imepangwa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa na miamba ya Tunisia Espérance Sportive de Tunis, Atlético Petróleos de Luanda ya Angola Pamoja na Stade Malien ya Mali. Droo ya Michuano hiyo imepangwa leo mchana Mjini Cairo, Misri. Hatua ya Makundi itaanza wiki ya tarehe 21–23 Novemba 2025, kwa siku mbili za mechi kuchezwa kabla ya kuanza kwa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies CAF Morocco 2025. Kisha shindano hilo litasitishwa na kuanza tena wiki ya tarehe 23-25 January 2026, huku awamu ya mtoano ikitarajiwa kuanza tarehe 13 Machi 2026. Aidha Bingwa wa CAF Champions League 2025/2026 atapata zawadi ya dola za Kimarekani 4,000,000, huku washindi wa pili watapata USD 2,000,000.
