YANGA Yapangwa Kundi B CAF Champions League 2025/2026
Droo ya hatua ya Makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League 2025/2026) imefanyika Leo Jumatatu tarehe 3 November 2025 huko Afrika Kusini. Klabu ya Yanga Katika droo hiyo imepangwa Kundi B Pamoja na miamba ya soka Afrika Ahly ya Misri. Timu nyingine ambazo zimepangwa Kundi B katika Droo iliyofanyika leo Mjini Cairo, Misri ni ASFAR ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria. Hatua ya Makundi itaanza wiki ya tarehe 21–23 Novemba 2025, kwa siku mbili za mechi kuchezwa kabla ya kuanza kwa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies CAF Morocco 2025. Kisha shindano hilo litasitishwa na kuanza tena wiki ya tarehe 23-25 Januari 2026. Awamu ya mtoano itaanza tarehe 13 Machi 2026. Aidha Bingwa wa CAF Champions League 2025/2026 atapata zawadi ya dola za Kimarekani 4,000,000, huku washindi wa pili watapata USD 2,000,000.
