Akielezea mashine na vifaa vinavyotumiwa na GST katika tafiti mbalimbali, Minja alisema kuwa GST ina mashine za kisasa, zikiwemo mashine za _magnetometer, mashine za GDD (ERT/IP) na ADEM Terrameter_ zinazotumika kubaini sifa za miamba na miamba yenye madini inayoonyesha kwa usahihi mwelekeo wa miamba yenye madini. PIA SOMA: Tarumbeta za GST kwa misalaba yake; ni bora kwa kuyeyusha sampuli za dhahabu “GST ni taasisi ya Serikali yenye jukumu la kufanya tafiti za madini nchini kwa zaidi ya miaka 100 sasa, kupitia tafiti hizo, GST imefanikiwa kukusanya taarifa nyingi za kijiosayansi katika maeneo mbalimbali nchini ambazo ni hazina kwa Taifa na wadau wa Sekta ya Madini. Akielezea hali ya tafiti nchini, Minja alieleza kuwa, hadi sasa GST imefanya utafiti wa kijiofizikia kwa asilimia 16, utafiti wa kijiografia asilimia 24, na utafiti wa jiolojia asilimia 98, hivyo amewataka wachimbaji madini nchini hususani wachimbaji wadogo kutumia taarifa hizo ili kuongeza uzalishaji wa madini na mapato yao kwa ujumla.
Tanzania yaagiza wachimbaji wadogo kukumbatia tafiti za kijiosayansi
By -
September 29, 2025
0
GEITA: Wachimbaji wadogo nchini wametakiwa kufanya tafiti za kijiosayansi katika maeneo yao ya uchimbaji kabla ya kuanza uchimbaji ili kubaini hali ya kijiolojia na uwepo wa madini hali itakayoongeza uzalishaji na kuleta tija ikiwa ni pamoja na kuepuka upotevu wa mitaji yao. Hayo yamesemwa leo na Mtaalamu wa Jiofizikia Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Jiolojia na Madini Tanzania (GST) Octavian Minja wakati akizungumza na viongozi wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (TAWOMA) waliotembelea banda la GST kwenye Maonesho ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Dk.Samia Suluhu Hassan, Bombambili, Manispaa ya Geita
Tags: